Picha na habari: Yaliyotokea kijijini Msimbati, Mtwara

Status
Not open for further replies.

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Ya awali ni maelezo ya Mhariri wa blogu ya ‘Kusini' na inayofuatia ni ya bwana Samli, wote wapo Mtwara, wanaripoti kuhusu taarifa za gari linalosadikiwa kuwa lilikuwa limeandaliwa kwenda kumchukua Bibi Somoye Issa (90) ambaye ni Mkuu wa Kaya aliyetoa kauli kuwa gesi ikisafirishwa kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam, itageuka kuwa maji, kuchomwa moto usiku wa jana huko kijijini Msimbati, Mtwara. Kijiji cha Msimbati ndicho ambacho miradi ya kuvuna gesi asilia imesimikwa.

511064662.jpg


Pichani juu ni Mhariri wa blog ya Kusini akitizama mabaki ya gari lililochomwa moto huko Msimbati.

785323387.jpg


Pichani juu Bibi Somoye Issa (90).


Kwa mujibu wa wanakijiji hao, Mtu huyo ambaye ana asili ya kijiji hicho waliyemtambua kwa jina la Seleman Babu aliwasili kijijini hapo jana saa 10 jioni akiwa na gari ndogo aina ya Mark II na kwenda nyumbani kwa shangazi yake.

Habari zinadai kuwa saa 2 usiku Babu, alikwenda nyumbani kwa Bibi Mtiti akiwa na gari pamoja na shangazi yake aliyetajwa kwa jina la Fatuma Saidi Tom.

Mkazi wa kijiji hicho, Juma Ayoub alisema: "Unajua yule bibi tunamlinda, sasa ilipoonekana ile gari usiku pale, watu wakaanza kujiuliza linafanya nini? Wakaanza kusogea, kadiri muda ulivyokwenda ndivyo watu walivyozidi kuongezeka."

Asha Hamisi, mtoto wa pili wa Bibi Mtiti, akihadithia juu ya tukio hilo alisema yapata saa 2 usiku wakiwa wanakula chakula alipokea wageni wawili ambao baada ya kumaliza kula waliomba kuongea na Mkuu huyo wa Kaya. "Alikuja kijana na mama wakaniomba kuongea na bibi... Alimuliza bibi kama ana uwezo wa kwenda Mtwara, bibi akajibu hawezi... Wakaniuliza mimi kama naweza kwenda badala yake nikawaambia siwezi... Akasema ametumwa na Rais Jakaya Kikwete na Hawa Ghasia wamjie bibi wakazungumze naye mambo ya gesi... Alisema kama bibi yupo tayari Jumanne ijayo watamfuata kwa gari, mimi nikasema sitaki, nilipochungulia nje nikaona watu wengi wamezunguka."

Manzi Mohamedi Faki mtoto wa tano wa Bibi Mtiti anasimulia: "Kwa kuwa tunamfahamu tulimwambia aondoke mpango aliojia haufai, akawa anabisha, tukaendelea kumsihi, wakati huo watu wanazidi kuongezeka, alipotoka akakosea njia, alipopita hakukuwa na njia, watu walimfuata wakaanza kumrushia mawe, aliacha gari akakimbia, ndipo wananchi walipoliteketeza gari kwa moto."

Fatuma Tom ambaye ni shangazi wa Babu amethibitisha kumpokea mwanae huyo na kumsindikiza kwa Bibi Mtiti na ambako alimuomba mkuu huyo wa kaya akubali kuondoka nae kwenda Dar es Salaam kwa maelezo kuwa ametumwa na viongozi wake wa juu: "Ni mwanangu mtoto wa kaka yangu, alikuja akaniomba nimepeleke kwa bibi akamsalimie tuliondoka saa 2 usiku…watu walituzingira na hali ilipokuwa mbaya niliondoka na kumwacha mwanangu pale, nae alikimbia na ndipo walipochoma moto gari.... Huyu mwanangu anaishi Dar es Salaam, anafanya kazi usalama wa Taifa…nadhani alirudi jana hiyohiyo Mtwara."

Mwenyekiti wa kijiji cha Msimbati, Salum Tostao alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa ofisi yake haikupokea mgeni yeyote kutoka serikalini kwa siku hiyo: "Ni kweli gari imechomwa lenye namba za usajili T 609 BXG mali ya Mussa Babu…taarifa hii ni kwa mujibu wa nyaraka tulizookota kutoka ndani ya gari hilo."

Selemani Babu alikanusha madai ya yeye kwenda kijijini hapo jana na alisema: "Hapana, hapana labda umekosea…na... na... na... umekosea… sijakwenda Msimbati jana… kwanini asiwe Mussa, umekosea sio mimi kwaheri."

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Maria Nzuki alisema hana taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo kwa kuwa mhusika hajaenda polisi kulalamika.

164661209.jpg


Pichani juu ni Aisha Hamisi ni mtoto wa pili wa Bibi Mtiti

520813565.jpg


Wananchi wakitizama mabaki ya gari lililochomwa moto

==========================

Baada ya majibizano ya hapa na pale kuendelea kwa muda mrefu baina ya Serikali, Wanaharakati na Wananchi wa Mikoa ya Kusini sasa inaonekana mgogoro huo kukua zaidi siku hadi siku. Ililipotiwa hapo kabla kuhusu Naibu Waziri wa Nishati kwenda usiku huko Msimbati na kufukuzwa, ingawaje Serikali kwa upande wake ilikanusha habari hiyo na kudai ni maneno ya kizushi na udanganyifu wa watu kujitafutia umaarufu.

Katika kile kinachoonekana kuwa ni hatari, asubuhi ya leo tumepata taarifa kwamba gari lililoenda kwa ajili ya kumbeba Bibi kwenda naye kusikojulikana limechomwa moto. Taarifa zinasema, watu kadhaa akiwemo kijana mmoja mwenye asili ya ukaazi wa kijiji hicho walikamatwa jana usiku na wanakijiji cha Msimbati wakidai wameagizwa kuja kumchukua Bibi huyo ili wakafanye maongezi na Wakubwa ambao pia hawakuweza kuwekwa bayana ni Wakubwa gani hao. Kinachoelezwa ni kwamba, baada ya mtafaruku huo, watu hao walichoropoka na kukimbia kitu kilichowapa hasira wananchi na kuamua kuchoma gali hilo ambalo walikuja nalo.

Wananchi hao wamesema wako tayari kumlinda Bibi huyo usiku na mchana kwa kuhofia kurubuniwa na Serikali ili abadili msimamo wake.

Ni hatari, kwa sababu mbali na propaganda za viongozi wetu wa Kitaifa kwamba suala la gesi ni la Wanamtwara Mjini tu; Kwamba wenyewe wa Msimbati na Mtwara Vijijini kwa ujumla wako tayari gesi hiyo kupelekwa Dar es salaam, si kweli. Leo hii, wale wanaodaiwa kuwa tayari kuruhusu gesi hiyo wameteketeza gari, je wale wasio tayari kwa hilo kesho watafanya nini?

Serikali isidharau wananchi na wale wenye matakwa mema na nchi hii, kwani mbali na mamlaka ambayo serikali imepewa katika kusimamia rasilimali za nchi, bado uhalali wa wamiliki asilia wa rasilimali hizo ambao ni wananchi hauwezi kuporwa. Wananchi wanaozungukwa rasilimali husika ndio wamiliki halali wa rasilimali hizo kabla ya Serikali na jamii zingine za nchi. Hivyo wanufaika wa kwanza wa rasilimali husika ni lazima wawe ni wale wenye uhalali wa Ki-asili na si vinginevyo.

Tuache dharau!

Leo gari limechomwa, kama hii hali itaendelea kuwa hivi, tusishangae kuambiwa kuna mtu pia kachomwa au kapoteza maisha kwa sababu hizi hizi zinazofanyiwa masihara na viongozi wetu.

Tuweni wazalendo, tutetee maendeleo ya nchi na watu wake kwa vitendo, tuache porojo.

---
Hassani Samli,
Mtwara.
samlihassani@yahoo.com

Source: wavuti.com
 
Tangu mwanzo nilijua haya madai yameambatana na ujinga ndani yake. Huu ndio uthibitisho wenyewe. Kama hako kabibi ni kachawi kiasi kanaweza kubadili hali ya vitu, kwa nini kasiibadili Mtwara iwe Durban?

Watu primitive namna hii wanataka maendeleo....!!
 
Safi sana!

Bhululu!
Wana Mtwara WADAI HAKI YAO BILA VURUGU;Sishabikii kamwe mambo haya!BIAFRA war kule Nigeria viliua watu wengi sana hasa watoto na akina Mama na vilianza hivi hivi kwa serikali na wakazi kugombania uhalali wa mchakato wa mali asili!

Kama tukishabikia vurugu JF tutakuwa watu wa ajabu kidogo na tutegemee akina Kanali Ojukwu wengine kuibuka Msimbati!
 
Bhululu!
Wana Mtwara WADAI HAKI YAO BILA VURUGU;Sishabikii kamwe mambo haya!BIAFRA war kule Nigeria viliua watu wengi sana hasa watoto na akina Mama na vilianza hivi hivi kwa serikali na wakazi kugombania uhalali wa mchakato wa mali asili!

Kama tukishabikia vurugu JF tutakuwa watu wa ajabu kidogo na tutegemee akina Kanali Ojukwu wengine kuibuka Msimbati!

Mkuu narudia tena safi sana,wakati mwingine kuna gharama ili kuipata haki
 
Tangu mwanzo nilijua haya madai yameambatana na ujinga ndani yake. Huu ndio uthibitisho wenyewe. Kama hako kabibi ni kachawi kiasi kanaweza kubadili hali ya vitu, kwa nini kasiibadili Mtwara iwe Durban?

Watu primitive namna hii wanataka maendeleo....!!

Wee weka ukada wako hapa wa maCCM, unamuita bibi KABIBI....yakikukuta mimi napita tu, heshima mbele jaribu nawewe kwenda kwake basiiii....
 
Wengine wakisema mpaka 'panya hawatabaki' mnashangaa...........Bibi Samoye Issa yeye ya kwake ni mafuta kubadilika na kuwa maji........anapata mpaka ulinzi wa hali ya juu huku TISS wakivinjari kupepesua.........Babu wa Loliondo, Mchungaji wa uongo Ambilikile Masapile, yeye ni kikombe na magonjwa yote yanapona...........mawaziri, maaskofu na watu wa rika tofauti kwa maelfu kama siyo malaki wanajazana kupata kikombe.

Hii ndiyo Tanzania ndani ya karne ya 21. We'll never be serious.
 
Komaeni,komaeni,komaeni!Mkicheka na nyani mtaambulia mabua.
 
Tangu mwanzo nilijua haya madai yameambatana na ujinga ndani yake. Huu ndio uthibitisho wenyewe. Kama hako kabibi ni kachawi kiasi kanaweza kubadili hali ya vitu, kwa nini kasiibadili Mtwara iwe Durban?

Watu primitive namna hii wanataka maendeleo....!!

Unachotakiwa kushangaa sio bibi kusema anaweza kugeuza gas kuwa maji, unatakiwa kushangaa viongozi wako wa serikali kuu kuamini kwamba bibi wakimrubuni kwa vijicent basi wanamtwara watamsikiliza bibi.

Dont miss the point here. Mkulu na viroboto ndo wanTakiwa tuwashangae.
 
Usalama wanataka kumpeleka bibi kwenye kale kamsitu kao kamateso! bibi ataweza kuvumilia kutoa jino bila ganzi? munge amuweke bibi mbali na ccm amen!!!! , amina!!!!
 
Tangu mwanzo nilijua haya madai yameambatana na ujinga ndani yake. Huu ndio uthibitisho wenyewe. Kama hako kabibi ni kachawi kiasi kanaweza kubadili hali ya vitu, kwa nini kasiibadili Mtwara iwe Durban?

Watu primitive namna hii wanataka maendeleo....!!

Mzee acha hasira, watu ni primitive kwa sababu ya serkali yako, hata wewe ni primitive tukikulinganisha na raia wa mataifa yaliyoendelea kama Japan, Germany nk, hako kabibi ni Tanzanian hero, Hana vifaru wala risasi kama ccm, kwa kutumia silaha pekee aliyo nayo ya itikadi za jadi ambayo wewe umeidhalau sana, bibi ameweza kusimama imara in defence of her God given natural resources licha ya ukweli kwamba yeye hataifaidi kulingana na umri wake, lakini ana matumaini wajukuu zake watafaidika, hii ndo inaitwa self sacrifice, historia itamkumbuka kwa ushujaa wake na wewe historia itakulaani kwa ujinga wako!
 
Jakaya hana haja na kuhangaika na wazee wa Mtwara. Awaite wazee wa Dar es salaam aongee nao ili mambo yaishe kama alivyozea. Ila hili limemshika pabaya kama hatakubali kupambana na ufisadi badala ya kuendelea kuupamba kama alivyozoea. Kila la heri ndugu zetu wa Ntwara mchike hapo hapo mchiachie wala kutichwa.
 
Serikali kuna inachotafuta, maana kama wananchi ambao ndio waajiri wakuu wa viongozi walio madarakani wameamua gesi isondoke Mtwara badala yake umeme uzalishwa Mtwara(which is logical) kwa nini serikali inakuwa na kiburi?Au kuna watu wameshavuta pesa ya ufisadi kwenye mradi wa ujenzi wa bomba sasaa wanaona ugumu kurudisha??Maafa yatakayotokea kusini serikali ya ccm (ambayo iliingia madarakani kwa hila) itawajibika.Wanafalsafa wanasema nchi iliyokaa kwa utuliza unaotokana na vitisho siku ikichafuka haitulii for many decades! keep watching!!!!
 
serikali iliyokosa weledi na umakini kiuongozi daima huonesha ombwe la uongozi kama hivi tunavoona sasa,ccm hali hii itakuja kuwagharim sana,na wategemee mengine mengi zaid ya haya,si weyewe wameyachokoza??na kurudi kwenye meza ya mazungumzo ili kubadilisha msimamo wao ccm hawataki,tutegemee mengine mengi tuh kutoka kusini.
 
Nadhani hii serikali pekee inayemuogopa mchawi na ni aibu serikali kutishiwa na mchawi. Hii inaonyesha viongozi wa juu wa serikali wanaamini na wanashiriki ushirikina mno. Halafu tukiambiwa watanzania tuko juu kwenye kushiriki uchawi eti tunabisha.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom