Manumba apelekwa Afrika Kusini kwa matibabu zaidi

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai, DCI, Robert Manumba, ameondoka jioni hii kuelekea Afrika Kusini, kwa matibabu zaidi baada ya hali yake kuwa nafuu kidogo.

Habari za uhakika zilizoifikia FikraPevu zimeeleza kwamba Manumba ameondoka kwa ndege maalum ya kampuni ya AAR kwenda Afrika Kusini akitokea hospitali ya Agakhan ya jijini Dar alikokuwa amelazwa baada ya kupelekwa Uwanja wa Ndege kwa gari la kubebea wagonjwa (ambulance) maalumu.

Kwa hisani ya Hali ya Manumba bado tete! Sasa akimbizwa Afrika Kusini… | Fikra Pevu
 
Haya mambo mbona yapo hivi, yani baada ya hali yake kuimarika ndo amepelekwa S.Africa.
 
Mwisho wa jeuri na kibri ni mauti....hapa ndipo usawa unapokuja. Kumbe polisi nao wana miili ya nyama? Wanaweza kuumwa na kamdudu km mbu wakapiga mweleka? Yako wapi mabomu ya machozi, risasi za moto kwanini msitumie silaha hizo km kinga?.
 
Dah!Mungu amsaidie apone haraka na arejee nyumbani kuendelea na ujenzi wa taifa.
 
Mwisho wa jeuri na kibri ni mauti....hapa ndipo usawa unapokuja. Kumbe polisi nao wana miili ya nyama? Wanaweza kuumwa na kamdudu km mbu wakapiga mweleka? Yako wapi mabomu ya machozi, risasi za moto kwanini msitumie silaha hizo km kinga?.

Nahisi ameshaonana na Mwangosi,kila mwanadamu ana damu,na atanuka akifa.Kumbe hata riafande rikubwa rinaugua.Mura,beba sana sote sa kasi,faa mabomu ya machosi,AK 95,RIVOLFA,SIRENT KIRA, muwe furu musunguke kire kitanda cha musee munumba mufukuse uchafu yote.
 
dua za sheikh ponda hizop zinammaliza,haoni mrema alisomewa al badir,mwili wote umekua na mabaka kama chui
 
Mkurugenzi wa Upelelezi wa
Jinai, DCI, Robert Manumba, ameondoka jioni hii kuelekea Afrika Kusini,
kwa matibabu zaidi baada ya hali yake kuwa nafuu kidogo.

Habari za uhakika zilizoifikia FikraPevu zimeeleza kwamba
Manumba ameondoka kwa ndege maalum ya kampuni ya AAR kwenda Afrika
Kusini akitokea hospitali ya Agakhan ya jijini Dar alikokuwa amelazwa
baada ya kupelekwa Uwanja wa Ndege kwa gari la kubebea wagonjwa
(ambulance) maalumu.

Kwa hisani ya
Hali
ya Manumba bado tete! Sasa akimbizwa Afrika Kusini… | Fikra
Pevu

Hii 'malaria' kiboko, hadi south?
 
Si ndio huko alipopelekwa kinara wa mgomo wa madaktari, Ndugu Ulimboka akapona?

Basi South good kuliko Apollo
 
Wapi Mwangosi(R.I.P)?Aaah!Kumbe na wao wanaogopa kufa?Mbona sasa hawaogopi kuua wenzao?...Hakyanani kumbe Duniani tunapita pamoja na Polisi?Mungu amua kwa haki usitupendelee wala usituonee maana wewe ni chemchem ya haki Aaaaamen
 
Back
Top Bottom