Vurugu Dumila: Polisi watumia Nguvu, barabara yafungwa kwa muda!

May 1, 2012
95
96
Kuna maandamano yamefanywa na wananchi eneo la Dumila.

Chanzo ni mgogoro kati ya WAKULIMA na WAFUGAJI. Makazi ya wafugaji yamechomwa moto.

Mpambano unaendelea wananchi wamebeba silaha za jadi wanaelekea kituo cha POLISI.

Wananchi wakulima wanamtaka Mkuu wa Mkoa wa Morogoro (Joel Bendera) kufika kuwatatulia tatizo lao la kunyang'anywa maeneo yao na kuwapatia wafugaji.

Wananchi hao wamegawanyika katika makundi kadhaa huku kila kundi likifunga barabara ya kuingia na kutoka eneo hilo la Dumila, ambapo wamezuia magari yote yanayopita eneo hilo kutoka Morogoro na kutoka Dodoma.

Tayari Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, ameomba udhuru kutoka katika Kikao cha wakuu wa mikoa, kilichokuwa kikiendelea mkoani Dodoma na yupo njiani akielekea eneo hilo kwa nia ya kukutana na wananchi hao ili kuwasikiliza na kutatua mgogoro huo.

Wafugaji wanapendelewa na mkuu wa wilaya na mapolisi kwa kuwa wanahonga sana.

Mgogoro wa eneo hilo na wilaya ya Kilosa kwa ujumla ni mkubwa sana na wa miaka mingi sana (Nilishawahi kufanya research huko 2003 kuhusu migogoro ya ardhi). Inashindikana kutatuliwa kwa kuwa wafugaji wana uwezo wa kuhonga wakati wakulima hawana uwezo wa kuhonga.

Kumbukeni mgogoro wa Msovero mwaka 2001 ambako watu zaidi ya 100 walikufa. Serikali ya CCM imekuwa ikumbatia hii migogoro bila kutafuta suluhisho la kudumu. Pia mapendekezo ya sheria ya ardhi ambayo yangemaliza kabisa migogoro hii ya wakulima na wafugaji yalikataliwa na wabunge wanaotokea maeneo ya wafugaji kwa kuwa ingewanyima haki ya kugeuza nchi nzima eneo la malisho.

Serikali ya CCM imeshindwa kuleta maendeleo na inashindwa hata kutatua migogoro ya ardhi. Shime watanzania tuikatae CCM

Updates zaidi soma -> Baada ya vurugu kubwa Dumila, hali bado tete wilayani Kilosa...
 
Kweli nchi hii haitawaliki kila kona vipigo na maandamano watu wanadai haki zao, na haki haiombwi inadaiwa kwa njia yeyote ile.
 
Tatizo ni chama tawala viongozi niwale wale wa zamani enzi za zidumu fikra sahihi za mwenyekiti.bila kujua wananchi sio wale .
 
jamani hali ni mbaya watu ni wengi polisi wameshindwa muda huu barabara ya Dodoma magari hayapiti mawe yamewekwa barabarani
 
Kumetokea kutoelewana kati ya wakulima na wafugaji baada ya mkuu wa wilaya kuwapa wafugaji haki ya eneo hilo na kuwataka wakulima waombe radhi kwa wafugaji.

Pia kwa sasa wananchi ndo wanaelekea kituo cha polisi.
 
maeneo ambayo toka zamani yalikuwa yanamilikiwa na wakulima leo hii wamepewa wafugaji sasa wananchi wamepinga na wameamua kuandamana
 
muda huu watu wanataka kwenda kuchoma moto kituo cha polisi magamba mnaimalza nchi
 
Kuna maandamano yamefanywa na wananchi eneo la Dumila.

Chanzo ni mgogoro kati ya WAKULIMA na WAFUGAJI. Makazi ya wafugaji yamechomwa moto.

Mpambano unaendelea wananchi wamebeba silaha za jadi wanaelekea kituo cha POLISI.
Msijali,huo ni upepo tu unapita, nchi yetu ni kisiwa cha amani na utulivu, ambapo hadi nchi jirani zinazotuzunguuka wanatuonea wivu!!!
 
Wafugaji wanapendelewa na mkuu wa wilaya na mapolisi kwa kuwa wanahonga sana.

Mgogoro wa eneo hilo na wilaya ya Kilosa kwa ujumla ni mkubwa sana na wa miaka mingi sana (Nilishawahi kufanya research huko 2003 kuhusu migogoro ya ardhi). Inashindikana kutatuliwa kwa kuwa wafugaji wana uwezo wa kuhonga wakati wakulima hawana uwezo wa kuhonga.

Kumbukeni mgogoro wa Msovero mwaka 2001 ambako watu zaidi ya 100 walikufa. Serikali ya CCM imekuwa ikumbatia hii migogoro bila kutafuta suluhisho la kudumu. Pia mapendekezo ya sheria ya ardhi ambayo yangemaliza kabisa migogoro hii ya wakulima na wafugaji yalikataliwa na wabunge wanaotokea maeneo ya wafugaji kwa kuwa ingewanyima haki ya kugeuza nchi nzima eneo la malisho.

Serikali ya CCM imeshindwa kuleta maendeleo na inashindwa hata kutatua migogoro ya ardhi. Shime watanzania tuikatae CCM
 
wilaya ya kilosa ni wilaya inayoongoza kwa ufisadi ndo maana haya yote yanatokea, sasa mtu mmja anasababsha uharibifu mkubwa wat wamejaza miti,mawe,machuma barabarani
 
Hizi ndizo athari za kula 'mlungula' kwa watawala wenye uwezo wa kutawala familia. Rejea kauli ya Mh. Kafulila aliyowahi kuitoa bungeni juu ya madhaifu ya watawala.
 
Kweli mwaka 2013 ni mwaka wa nguvu ya umma.Thats great,keep on pressing people's power.
 
Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom