Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,393
Suala la mwanamke kuzaa pasipo kuolewa sio geni siku hizi. Kuna wimbi kubwa la wanawake waliozaa bila kuolewa. Si lengo langu kuzungumzia sababu ya uwepo wa wanawake waliozaa bila kuolewa, lakini ninachotaka tujadili hapa ni swala la mwanamke kumtambulisha mpenzi mpya kwa mzazi mwenzie.
Inaweza kutokea kwamba mwanamke amezaa na mwanaume lakini kutokana na sababu fulani fulani, swala la kuoana likashindikana. Lakini mwanaume huyo anawajibika kwa malezi ya mtoto na anakwenda kumuona mtoto mara kwa mara na hata kutumia muda hapo nyumbani kwa mwanamke akicheza na mtoto au kumchukua mtoto na kwenda kushinda naye kwake na kisha kumrudisha kwa mama yake.
Kwa kuwa uhusiano wa kimapenzi haupo tena, huyu mwanamke anapata mpenzi mpya ambaye wanaanza uhusiano wa kimapenzi.
Mwanamke, hebu niambie:
1. Je unadhani ni vyema kumkutanisha mzazi mwenzio na mpenzi wako mpya kwa ajili ya utambulisho mwanzoni mwa uhusiano wako na huyo mpenzi mpya?
2. Je unadhani mpenzi wako mpya atauchukuliaje uhusiano wako wewe na mzazi mwenzio linapokuja swal la malezi ya mtoto?
3. Je utamthibitishiaje mpenzi wako mpya kwamba hutarudiana na mzazi mwenzio na kumtelekeza, iwapo mtamaliza tofauti zenu?
Hebu wana JF nipeni uzoefu wenu katika jambo hili……….