Joyce Ndalichako: Clouds FM ilimpa promo kijana aliyendika matusi kwenye mtihani wa Kidato cha Nne

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,028
144,382
attachment.php

Katibu mkuu wa baraza la mitihani la taifa, Bi Joyce Ndalichako, amekilaumu kituo cha Radio cha Clouds FM kuwa kilimpa promotion kijana aliendika matusi na "Bongo Flavor" katika mtihani wake wa Kidato cha Nne Mwaka jana kwa kumfanyia interview katika moja ya vipindi vyake.

Katibu mkuu huyo amedai kuwa hatua hiyo ya Clouds FM imechangia uandikaji wa matusi kwa watahaniwa wa mwaka huu.

Hata hivyo, watangazaji wa kituo hicho wamepinga vikali kauli hiyo na badala yake wamemtaka katibu mkuu huyo atoe sababu za kisayansi za kufeli kwa wanafunzi.

Source: Clouds FM asubuhi ya leo.

=================================

Updates

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Joyce Ndalichako akionyesha karatasi ya majibu ya mmoja wa watahiniwa wa mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2012, Dar es Salaam jana. Picha na Edwin Mjwahuzi

Posted Jumanne,Februari19 2013 saa 20:52 PM

KWA UFUPI

"Unakuta mwanafunzi anaeleza anavyolishangaa Bunge… mtu anaandika… nawashangaa wabunge, wamekaa kama wapo kijiweni, wabunge wamekosa ustaarabu, badala kujadili

Fredy Azzah, Joyce Mmasi

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inaweza kukumbwa na kashfa kubwa kutokana na matokeo mabaya ya kidato cha nne ya 2012 yaliyotangazwa juzi na Waziri wake, Dk Shukuru Kawambwa.

Kashfa hiyo inatokana na aina ya majibu yaliyoandikwa na baadhi ya watahiniwa katika mitihani hiyo, huku wengine wakikusanya vitabu vya majibu bila kujibu chochote, hali inayohusishwa na uhaba mkubwa wa walimu katika baadhi ya shule za sekondari nchini.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk Joyce Ndalichako alisema wasahihishaji walikutana na mambo ya ajabu yakiwamo matusi, michoro ya vitu visivyoeleweka, mashairi na nyimbo za muziki wa kizazi kipya (bongo fleva).

"Mwaka jana tulikutana na ‘single' yaani waliandika mashairi kwa uchache, lakini mwaka huu tumepata albamu nzima… ni vituko vitupu, wengine wanaandika mapenzi, mwanafunzi anatumia ukurasa mzima kumlalamikia mpenzi wake. Miongoni mwa yaliyoandikwa ni mpenzi, umeniacha, natamani kunywa sumu, usiku silali nakuwaza wewe…" alisema Dk Ndalichako.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili ofisini kwake Dar es Salaam jana, Dk Ndalichako alisema wanafunzi wengine waliandika malalamiko dhidi ya wabunge na uendeshaji wa Bunge.

"Unakuta mwanafunzi anaeleza anavyolishangaa Bunge… mtu anaandika… nawashangaa wabunge, wamekaa kama wapo kijiweni, wabunge wamekosa ustaarabu, badala kujadili kero za wananchi waliowachagua, wanapokea timu zilizoshinda makombe… timu ikishinda Kombe la Kagame inapokelewa bungeni. Bunge limekuwa kama kijiwe, bungeni siyo ukumbi wa starehe kama mnataka kupokea timu hizo nendeni katika ofisi zao au viwanjani…" alisema.

Alisema wanafunzi walioandika vitu visivyoeleweka walikuwa ni wengi na walichangia kwa kiasi kikubwa matokeo kuwa mabaya.

Dk Ndalichako alionyesha baadhi ya michoro hiyo ambayo inaonyesha vikaragosi ambavyo wanafunzi hao waliviita Messi (Lionel, mchezaji wa Barcelona) na zombi (ni picha za kutisha) ambazo huonyeshwa kwenye televisheni.

Sababu za kufeli
Dk Ndalichako alisema hawezi kuwa na jibu la moja kwa moja juu ya kwa nini matokeo ya mwaka huu yamekuwa mabaya, lakini akadokeza kuwa huenda yametokana na wanafunzi wengi kukosa maarifa.

Anasema mbali na waliojaza matusi na michoro, wanafunzi wengine waliofanya vibaya ni wale ambao hawakujaza chochote kwenye karatasi zao za majibu.

"Kuna baadhi ya shule unakuta darasa zima watoto hawajajibu somo fulani kwa mfano Biolojia, wanaingia tu na kuandika namba. Tuliamua kuwapigia simu walimu wao, majibu waliyokuwa wakitupa ni kuwa hawajawahi kuwa na walimu wa somo husika kwa hiyo watoto hawakuwa na cha kujaza."

Dk Ndalichako alisema kwa ku mbukumbu zake, hakuna matokeo mabaya kama ilivyo kwa mwaka huu yaliyowahi kutokea.

"Tukiangalia tu kuanzia 2000, hakujawahi kutokea matokeo mabaya kama haya, kwa kweli hali haipendezi. Hata kabla ya kuyatangaza nilikuwa nayaangalia mara tatu tatu, sikuyapenda na inasikitisha kwa kweli," alisema Dk Ndalichako.
 
Clauds ina cha kujibu juu ya mambo mengi mabaya yanayotokea hapa nchini. Mara nyingi mnashabikia yasiyofaa na hasa kuunga chama cha magamba ili hali mwajua ndio the big founder wa kila jambo likiwemo la matokeo mabaya ya kidato cha nne. Leo shule za msingi. wamechukua hadi alama70 je wategemea kidato cha nne watafanya nini?
 
Hata hivyo, watangazaji wa kituo hicho wamepinga vikali kauli hiyo na badala yake wamemtaka katibu mkuu huyo atoe sababu za kisayansi za kufeli kwa wanafunzi.

Ina maana elimu waliyonayo haiwatoshi kutambua ya kwamba sio kazi ya NECTA kutoa sababu za kufeli kwa wanafunzi. NECTA wanatunga maswali, wanasahihisha, wanatoa matokeo. Labda wawe wametunga maswali nje ya mitaala (mibovu iliyopo)
 
Mkuu hapo kwenye RED, si tumeambiwa hivi karibuni kwamba Tanzania hakuna mitaala, na ile iliyowasilishwa bungeni ilikuwa ni feki?

Tiba
 
Necta wangeachia mithihani iibiwe, pia mgewalaumu .... wamebana matokeo ndio hayo
 
Mkuu hapo kwenye RED, si tumeambiwa hivi karibuni kwamba Tanzania hakuna mitaala, na ile iliyowasilishwa bungeni ilikuwa ni feki?

Tiba
Mkuu mitaala ipo ila ni ya zamani na haifai kabisa kwa sasa. Wakati nasoma O'level nilishawahi kuuona, labda ndio huo feki ila ni zamani kidogo!
 
Kwa ujumla bongo fleva inaharibu society kuliko kujenga. Vituo vya redio na tv vinapropagate huu ujinga kwa nguvu kubwa kutoa platform na ku-encourage vijana kua 'wanamziki' na kupenda mziki zaidi kuliko kua na 'real job' itayocontribute kwene uchumi wa nchi. Lakini dhambi hii ni ya jamii nzima, si CLouds peke yake. Kila mtu ajiangalie/
 
Hata mimi nimesikiliza hii redio napata hofu kubwa na mashaka juu ya hawa watu sijui kama wanafikiria vizuri maana unamsikia mtu anaongea upuuzi mpaka unataka kutapika. Hivi NECTA inawezaje kueleza kwa nini wanafunzi wamefeli shame on this mbulula HONDA
 
Ina maana elimu waliyonayo haiwatoshi kutambua ya kwamba sio kazi ya NECTA kutoa sababu za kufeli kwa wanafunzi. NECTA wanatunga maswali, wanasahihisha, wanatoa matokeo. Labda wawe wametunga maswali nje ya mitaala (mibovu iliyopo)

mbali sana kwa clouds, hawawezi kufika
 
Katibu mkuu wa baraza la mitihani la taifa,Bi Joyce Ndalichako,amekilaumu kituo cha radio cha cluods FM kuwa kilimpa promotion kijana aliendika matusi na "bongo flavour"katika mtihani wake wa kidato cha nne mwaka jana kwa kumfanyia interview katika moja ya vipindi vyake.Katibu mkuu huyo amedai kuwa hatua hiyo ya Clouds FM imechangia uandikaji wa matusi kwa watahaniwa wa mwaka huu.

Hata hivyo, watangazaji wa kituo hicho wamepinga vikali kauli hiyo na badala yake wamemtaka katibu mkuu huyo atoe sababu za kisayansi za kufeli kwa wanafunzi.

Source:Clouds FM asubuhi ya leo.

Ndalichako unasahau kuwa hicho kituo ni option ya TBC1.
 
Kwa ujumla bongo fleva inaharibu society kuliko kujenga. Vituo vya redio na tv vinapropagate huu ujinga kwa nguvu kubwa kutoa platform na ku-encourage vijana kua 'wanamziki' na kupenda mziki zaidi kuliko kua na 'real job' itayocontribute kwene uchumi wa nchi. Lakini dhambi hii ni ya jamii nzima, si CLouds peke yake. Kila mtu ajiangalie/

Mkuu heshima kwako,kweli kabisa huu uvivu ndio unapelekea hivyo,vijana wanawaza kazi nyepesi tu na hakuna wanachoona chepesi kama bongo flava,
 
Hoja ya nassari labda ingekuwa na vipengele vya suluhisho la matatizo haya, pia hoja ya Mbatia ingetupa mwangaza tosha... lakini bunge letu likaona hazina maana namlaumu sana Ndugai kwa hili. pia ikumbukwe kwamba Elimu ya tz ilianza kuharibiwa kipindi cha waziri mungai. tusimshutumu kawamba Rais anatakiwa kumtafuta refomist tuanze moja tena anatakiwa mtu anaeijua vizuri hiyo wizara na mwenye mlengo wa mabadiliko. tukiacha siasa tukajikita kwenye kutafuta njia tutafika.
 
Back
Top Bottom